Imamu Husein (a.s) pamoja na wafuasi wake pale walipokuwa Karbala, walikuwa wakisoma mashairi maalumu yenye ibara za kivita, kwa ajili ya kuwahamasisha wanavita, pia Abul-Fadhlil-Abbaas alionekana mara zote katika siku ya Ashura kusoma aina mbali mbali za ibara na mashairi ya kuvutia kwa ajili ya uhamasishaji, mashairi yake yalikuwa ni jambo moja muhimu lililoweza kuwapa moyo wa ushupavu wanajeshi wa Imamu Husein (a.s) na hasa hasa watu wa famila Yake (a.s) wakiwemo watoto wadogo. Baadhi ya mashairi aliyokuwa akiyasoma baada kufikwa na madhila mbali mbali, ni kama ifuatavyo:
Pale watoto wadogo walipodatisha ukulele wa kutaka maji kutokana na kiu kali iliyowakumba, Imamu Husein (a.s), alimuamuru Abul-Fadhlil-Abbaas aelekee kwenye mto wa Furaat kwa ajili ya kuleta maji, mto ambao ulikuwa umezingiwa na jeshi la watu 4000, kwa ajili ya kumzuia Imamu Husein na wafuasi wake (a.s) wasipate maji, Abul-Fadhlil-Abbaas aliuelekea mto huo huku akisoma mashairi yafuatayo:
أُقاتِلُ القومَ بقلبٍ مُهتَدى اَذُبُّ عَن سِبطِ النبىِّ احمد...
Maana yake ni kwamba: napambana nanyi enyi watu kwa moyo ulioongoka * namtetea mjukuu wa Ahmadi mtume wetu hakika.
Aliendelea kutumia ibara zenye kuvutia akisema: nitavitwanga vichwa vyenu kwa upanga mkali, mapigano yangu yaliojawa na furaha yataendelea hadi mtapotengana na Husein (a.s)! mimi ni Abbaas mwana wa Ali Murtadha (aliyeridhiwa na Mola wake) ambaye alikuwa akithaminiwa na Molawe. Yeye aliwatawanya wafuasi wa Yazid kutoka kuliani na kushotoni mwake huku akiwacharaza upanga, alifanya hivyo huku akitiririka mashairi yasemayo:
لا أَرهبُ الموتَ إذا الموتُ زَفا
حتى أوارى فى المصالیت لقا
إِنّى اَنَا العباس اغدُو بالسِّقاء
ولا اَهابُ الموتَ یومَ المُلْتَقى
Maana yake ni kwamba: mimi siyaogopi mauti yenye kuondoa uhusianno baina yangu na mwili wangu, na wala sitayachelea hadi pale nitapouona mwili wangu umeshaanguka pamoja na mashujaa kwenye ardhi, mimi ni Abbaas ambaye kazi yangu ni kuwanywesha wenye kiu, na si mwenye kuogopa mauti pale nikiwa mapambanoni. Hapo akwa yeye tayari ameshaufikia mto Furaat, akanyosha mkono wake ili anywe maji, lakini alipozitafakari kiu za wengine aliamua kutoyaonja maji hayo, hapo akasoma mashairi haya:
یا نَفسُ مِن بعدِ الحُسین هُونى
مِن بعده لاکُنتِ اِنْ تَکونى...
هذَا الحسین وارِدُ المَنونِ
و تَشْرَ بینَ بارِدَ المعین
تاللّه ما هذا فِعالُ دینى
Maana yake ni kama ifuatavyo: ewe nafsi nyong’onyea usimtangulie Husein wala usiishi baada yake, hivi wewe unataka kunywa funda la maji hali akiwa Husein anapiga mafunda ya mauti! Kwa kweli mimi siwezi kufanya hivyo, hichi si kitendo kinachoweza kutendwa na nami wala na muungwana yeyote yule. Baada tu ya kusoma mashairi hayo, mvua ya mishale ikaanza kummiminikia, kisha Zeid bi Waqaar akamvamia na kumkata mkono wake wa kulia, hapo Yeye akaushika upanga wake kwa mkono wa kushoto huku akisoma mashairi yafuatayo:
واللّه إِن قَطَعْتُمُوا یَمِینى
إِنِّى اُحامى اَبَدا عَن دینى...
وَ عن امامِ صادِقِ الیَقینِ
نَجْلِ النَّبِىِّ الطاهِرِ الأمین
Maana yake ni kwamba: naapa kwa Mola ya kwamba, iwapo mtaukata mkono wangu wa kulia, bado mimi sitoacha kuihami dini yangu, mimi sitoacha kumhami Imamu wa kweli mwenye yakini, ambaye ni mwana wa mtume mwema aliyetoharika. Hizi ni baadhi ya tajo na mashairi aliykuwa akiyasoma huko Karbala, amma kuhusiana na swali lisemalo kuwa je yeye alipiga takbira pale alipokuwa akipambana na adui zake? Kwa kweli sisi hatukubata rejeo zozote zile zenye kuashiria jambo hilo, lakini si jambo geni kusikilikana sauti za takbira katika vita hivyo, kwani takbira ilikuwa ndiyo utajo maarufu mbele ya wafuasi wa Imamu Husein (a.s), pia wao walikuwa wakiutaja utajo wa "لاحول ولا قوة الا بالله" kila mara, na pia si jambo geni kusikilikana sauti kama hizo kutoka upande maaadui, kwani madai ya vita vyao dhidi ya Imamu Husein (a.s), yalikuwa ni kupagana na wale waliotoka katika misingi ya sheria za Kiislamu, na huo ndio uvumi walikuwa wakiuvumisha katika pande tofauti za jamii, walifanya hivyo ili kuwazubaisha wale wasiofahamu, na kuutambua Uislamu kisawasawa.