advanced Search
KAGUA
8706
Tarehe ya kuingizwa: 2010/03/16
Summary Maswali
je Imamu Khomeiniy (r.a) alikuwa anaamini kuwa kuadhimisha kwa kilio na maombolezo siku ya kuuwawa Imamu Husein (a.s), ndiyo sababu iliyoufanya Uislamu kubaki hai na imara tokea zama za Maimamu (a.s) hadi leo? Na kama alikuwa na imani hiyo, basi ni kwa msingi gani?
SWALI
je Imamu Khomeiniy (r.a) ana kauli isemayo kuwa: kulia na kuomboleza ndani siku ya maadhimisho ya kuuwawa kwa Imamu Husein (a.s), ndiyo sababu zilizosababisha Uislamu kubaki hai hadi leo? Na usemi wake huo umesimama kwenye msingi na dalili gani?
MUKHTASARI WA JAWABU

Imamu Khomeiniy (r.a), alitilia mkazo sana katika mazungumzo yake ya mara kwa mara ya kwamba: muhanga wa Imamu Husein (a.s), pamoja kuadhimisha siku ya muhanga huo kwa kuandaa vikao vya maombolezo kwa ajili ya kuikumbuka kwa ajili ya kupata somo juu ya tendo hilo la Imamu Husein (a.s), ni jambo linalopaswa kupewa umuhimu na kuhifadhiwa, kwani jambo hilo ni moja kati ya mambo yenye kupiga vita miporomoko mbali mbali ndani ya dini na jamii. Moja kati ibara za Imamu Khomeiniy (r.a) kuhusiana na hilo ni ibara isemayo: “Mkusanyiko wa kuadhiisha tokeo la Ashura kwa njia ya maombolezo maalumu juu ya mashahidi wa Karbala, ni jambo lenye kuleta Baraka nyingi’.[1] Pia alilisisitiza suala hilo kwa kusema: “Mwezi wa Muharram na Safar, ni miezi yenye baraka, miezi ambayo Uislamu umehuika ndani yake, ni wajibu kwetu sisi kuihuisha miezi hii kwa kuomboleza kutokana na misiba ya watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), kwani maombolezo hayo ndiyo yalioweza kuyadumisha madhehebu ya Ahlul-Bait (a.s) hadi leo. Miezi ya Muharram na Safar ndiyo iliyoupa uhai Uislamu huu. Muhanga wa Sayyidu Shuhadaa (bwana wa mashaidi) (a.s), ni suala moja kuu lililotuokolea dini yetu hadi leo… .[2]

Imamu komeiniy alikuwa akilizungumzia suala hilo ndani ya hutuba zake tofauti, huku akitoa dalili juu ya usemi wake huo, hebu basi tuiangalie hutuba yake isemayo hivi: “ Ndani ya siku za Ashura, au ndani ya mwezi wa Muharram na Safar na pia ndani ya mwezi wa Ramadhani, maadui huwa na khofu ya kuulembea Uislamu maneno ya fedheha na ufedhuli, au kutaka kuivuruga jamii ndani ya masiku kama hayo. Hii inatokana na wao kutambua kuwa ndani ya siku hizo na miezi hiyo, Waislamu huwa wapo chini ya bendera moja ya ibada na maombolezo, huku wanachuoni mbali mbali wakiihudumia jamii kwa kuipa nasaha muhimu, hivyo basi wao wanatambua kuwa: iwapo watataka kuichafua jamii, wanachuoni hao hawatokaa kimya, bali watawazindua wanajamii hao kuhusiana na njama hizo, na hatimae njama zao zitafedhehewa. Wao wanatambua kuwa mikusanyiko ya watu wanao omboleza kifo cha Imamu Husein (a.s), ni mikusanyiko yenye mfumo maalumu wa mshikamano wa sauti moja, watu hao wanapo omboleza mauwaji ya Karbala, damu zao huwa zinawachemka kwa hasira juu ya tokeo hilo, nao huwa na shauku kubwa ya kutaka kuitetea dini yao kama vile Imamu Husein (a.s) pamoja na wafuasi wake walivyofanya. Hivyo basi iwapo kutatokea machafuzi na dhulma ndani ya dini na jamii yao ndani ya wakati huo, wao watakuwa tayari kujitoa muhanga na kuitetea dini na jamii yao. Ndani ya miezi hiyo huwa hakuna haja ya kuwakusanya watu na kuwapigia bomba, bali makundi mbali mbali ya watu ndani ya mikoa mbali mbali, huwa yako tayari kwa ajili ya kupokea ujumbe maalumu kutoka kwa wanazuoni wao. Mmoja kati ya Maimamu (a.s), nafikiria kuwa alikuwa ni Imamu Baaqir (a.s), alikuwa akisema: “Nileteeni mtu wa kunisomea taazia (maombolezo) kwa ajili ya Karbala, ili asome na alie mbele yangu… . Imamu Baaqir hakuwa akifanya hivyo kwa ajili ya malengo ya nafsi yake, bali Yeye (a.s) alikuwa na malengo maalumu ya Kisiasa yaliolenga kuifufua na kuijenga jamii. Wengi miongoni watu waliojisinga (waliojipaka) rangi ya Umagharibi, wanatucheka na kuiita jamii yetu kuwa ni (jamii ya waliaji ovyo), lakini si wao tu bali hata wale watu walio karibu yetu, hawakijui ni kiasi gani cha thawabu anachokipata  yule anayewalilia kwa huzuni mashahidi wa Karbala. Wao hawajui kiwango cha thamani ya maombolezo haya, wala hawatambui thamani ya dua zinazo ombwa kwenye vikao hivyo. Vikao hivi ni mfumo maalumu wa kuwakusanya Waislamu na kuwaweka kwenye lengo moja, jambo ambalo huwafanya wao kuwa ni kundi moja kubwa la wanajeshi wa kuitetea dini na haki za wanajamii mbali mbali. Mkusanyiko wa aina kama hiyo huwa una malengo makubwa ya Kisiasa yenye kuwafanya watu kukielekea kitu kimoja muhimu juu yao chenye makusudio ya utetezi wa dini na jamii. Watu wanapokusanyika na kuomboleza, huwa wanapata muamko maalumu wa Kisiasa wenye kuwafumbua macho, na hilo ndilo lengo la Maimamu (a.s) katika kudumisha vikao hivi vya maombolezo, na wala hakutoweza kupatikana jambo litakalowaamsha Waislamu kuliko jambo hili. Wairani walipoamua kuiangusha serikali ya kidhalimu, walivitumia vikao hivyo kuwa ndio nyenzo muhimu ya kuwahamasisha wana jamii na kuwataka wasimame kidete juu ya utetezi haki zao, na wangelikuwa wao hawakupikika vizuri ndani ya chungu cha maombolezo hayo, basi ingelikuwa ni vigumu sana kuweza kufaulu katika mapinduzi yao, kwani wao walihujumiwa kutoka kila pembe, lakini kumbukumbu ya tokeo la Karbala ikawa ndio ngao ya fikra zao kusonga mbele na hatimae kuzifikia nyanja za juu za maendeleo ya Kisiasa na Kiufundi. Vijana wa Kiirani walipofahamu kuwa Imamu Husein (a.s), alijitolea muhanga yeye pamoja na familia yake kwa ajili ya dini na kwa ajili ya kupata ridha ya Mola wao, vijana hao walisonga mbele bila ya woga katika vita vya Sadamu Husein dhidi ya Iran, vijana hao walikuwa na shauku kubwa ya kufa shahidi kama alivyouwawa Imamu Husein (a.s) pamoja na wafuasi wake, jambo ambalo liliwafanya wao wasonge mbele bila ya khofu, na pale mmoja wao alipokuwa hakufanikiwa kufa shahidi, alikuwa akilia na kuhuzunika kutokana na hilo, wazee pia nao walikuwa wakiona fakhari pale waliposikia kuwa mmoja kati ya watoto wao amekufa shahidi, wazazi hao waliposikia kifo cha mtoto wao, bado walikuwa hawarudi nyuma, bali walikuwa wakisema: bado tuna mtoto mwengine, na kama kutahitajika wanajeshi, basi sisi hatuna upinzani juu ya hilo, na watoto wenyewe nao walikuwa na hamu ya kushiriki vita hivyo. Hivyo ndivyo vikao vya dua na maombolezo vinavyoijenga jamii, na suala hilo ni moja kati ya misingi mikuu iliyojengwa na Uislamu tangu mwazo, kwa ajili ya kuihifadhi jamii ya Waislamu. Ni muhimu watu kuufahamu umuhimu wa maombolezo, na faida zinazopatikana ndani ya maombolezo hayo, pia wao wanatakiwa kufahamu kuwa: ni jambo gani hasa lenye kuvifanya vikao kama hivyo kuwa na umuhimu wa hali ya juu kama hiyo? Wale wajinga wangeliufahamu umuhimu na uhakika wa hilo, basi wasungetuita sisi kuwa ni (kaumu ya waliaji), bali wangelituita kuwa ni (kaumu ya wana hamasa). Watu wangeliufahamu uhakika wa dua za Imau Sajjaad (a.s)  zilizomo ndani ya kitabu (Sahifatu-Sajjaadiyya), na vipi dua hizo zilivyoweza kuleta mageuzi mbali mbali  ya Kisiasa, pia jinsi ya dua hizo zinavyoweza kumjenga mja kiimani na kifikra, basi wasingetuuliza sisi: ni kwa nini tosome dua? Kwani dua hizi zina umuhimu gani? Jamii yetu ni lazima ifahamu umuhimu wa vikao hivi, vikao hivi ndivyo vinavyoipa uhai jamii yetu na jamii za wenzetu. Enyi wanajamii msiache kusimamisha aina hii ya vikao, ndani ya Muharram, na msiache kusoma aina mbali mbali za dua ndani ya kila wiki, kwani watu wangelikuwa wanafahamu umuhimu wa dua na vikao hivyo! Basi hata wale waliojisinga (waliojipaka) rangi ya Umagharibi pia mngeliwaona wanahudhuria vikao vyenu, mimi nina matuaini kwa wanajamii wangu kuvitunza na kuvikozesha rangi zaidi vikao hivi… .[3] Mwisho wa kunukuu.

Kwa ajili ya kupata ufafanuzi zaidi kuhusiana na mada ya maombolezo ya Karbala, unaweza kuangalia vitabu husika vyenye kuzungumzia mada na faida za maombolezo ya Karbala.

 


[1] Sahifeye Imamu, juz/13, uk/326, chapa ya Tandhiim wa nashr aathaa Imamu Khomeiniy, Tehran, chapa ya nne ya mwaka 1386 Shamsia.

[2] Rejeo iliopita, juz/15, uk/330.

[3] Rejeo iliopita, juz/16, uk/344 hadi 348.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MASWALI KIHOLELA

  • je majini na Malaika walikuja kumsaidia Imamu Husein (a.s) pale alipokuwa vitani huko Karbala? Na kama wao walikuja kumsaidia, basi kwa nini yeye aliukataa msaada huo?
    12278 تاريخ بزرگان 2012/05/23
    Kuna baadhi ya Riwaya na Hadithi zilizopokelewa kutoka kwa baadhi ya Maimamu (a.s) zenye kuashiria suala hilo. Lakini hakuna ajabu kuhusiana na suala hilo, kwani Mwenye Ezi Mungu aliwanusuru mitume tofauti pamoja na mawalii wake kwa kuwapelekea msaada wa majini na Malaika, kwa hiyo hilo ...
  • kwa nini tuwe wakalidi (wafuasi)?
    7750 Sheria na hukumu 2012/05/23
    Ruhusa ya kumfuata ulamaa maalumu katika matendo ya ibada za kila siku, inatakiwa kutolewa na akili ya mtu mwenyewe. Na wala ruhusa hiyo haingojewi kutoka kwa Maulamaa, huku kila mmoja akielewa umuhimu wa suala hili ndani ya maisha yake ya kila siku. Katika hali yakawaida, ...
  • nini maana ya itikafu
    19422 Tabia kimtazamo 2012/05/23
    Neno (itikafu) kilugha, huwa lina maana ya kule mtu kukaa na kubaki katika sehemu au pahala maalumu, huku akiwa ameshikamana na jambo maalumu ndani ya mahala hapo, lakini neno hili kitaalamu (kwenye fani ya sheria za Kiislam) linamaanisha kule mtu kukaa katika sehemu takatifu kwa ajili ya ...
  • nini hukumu ya kupiga sindano ya nguvu au kutia maji ya nguvu (Intravenous injection) mwilini ndani ya Ramadhani?
    10005 Sheria na hukumu 2012/05/23
    Wanazuoni wamekhitalifiana kuhusiana na suala hilo. Kwa kupata jawabu tosha, ni lazima utuambie kuwa wewe ni mfuasi wa mwanazuoni gani? Ili tuweze kukupa jawabu makini zaidi. Kwa vyovyote vile mitazamo ya baadhi ya wanazuoni wetu ni kama iuatavyo: Bahjat (r.a) na Khameneiy (Mungu amuhifadhi), wanasema: ...
  • je Imamu Huein (a.s) aliwahi kuwa na bint aliyeitwa Ruqayya?
    7963 تاريخ بزرگان 2012/05/23
    Katika tokeo muhimu la Karbala, kulikuwa kuna aina nyingi za nyuso zilizong’ara, na baadhi ya nyuso hizo zilikuwa ni nyuso za watoto wadogo, lakini Tarehe haikunukuu habari kamili kuhusiana na nyuso zote za watoto hao. Lakini mmoja miongononi mwa watoto waliotajwa na Tarehe, ni Ruqayya mwana wa ...
  • ni sharti gani sahihi za utumiaji wa vitu au neema zilizomo ulimwenguni?
    9711 Tabia kimatendo 2012/06/17
    Uislamu haukuyazingatia mahitajio ya mwanaadamu kwa upande mmoja tu, kama vile zilivyo fanya dini nyengine, kwani dini nyingi ima hugharamika katika kuyazingatia mahitajio ya kiroho peke yake, au mahitajio ya kilimwengu tu. Uislamu umeshika njia ya kati na kati, na mtizamo wa Uislamu ni kwamba: kufaidika na ...
  • je mtu asiwajibikiwa kufunga (asiyefunga) ana ulazima wa kutoa zakatul-fitri?
    10872 Sheria na hukumu 2012/05/23
    Mtu atakaeingiliwa na usiku wa Idil-fitri, huku akiwa ni baleghe na mwenye akili timamu, naye akiwa si mtumwa wa mtu wala si fakiri, mtu huyo atawajibika kutoa zakatul-fitri kwa ajili yake na kwa ajili ya wale wote anaowahudumia, na kiwango cha kila mmoja ni kiasi cha kilo ...
  • ni zipi funga zilizo zisizofaa kwa mtazamo wa imam Shafi, Hanafi na Maalik?
    14429 Sheria na hukumu 2012/05/23
    Masiku yasiyofaa kufunga saumu mbele ya imam Abu Hanifa ni: siku ya idi ndogo na idi kubwa, pia kufunga siku ya mwezi 11, 12 na 13 ya mwezi wa Dhil-hijja, pia kufunga ndani ya idi pili hadi nne za idi ya mfunguo tatu. Funga zisizofaa ...
  • Niyə müsəlman bir kişi əhli kitab qadını ilə daimi evlənə bilməz amma müvəqqəti evlənə bilər?
    6530 Sheria na hukumu 2015/06/02
    Kitab əhli qadınları ilə müsəlman kişilərin daimi evliliyi barədə fəqihlərin baxışı müxtəlifdir. Bu ixtilafın səbəbi bu sahədə olan müxtəlif rəvayətlərdən irəli gəlir. Belə nəzərə çarpır ki, bəzi hədislərdə bu evliliyə icazə verlməməsinin hikməti müsəlman kişilərin kafir qadınların əxlaq və xasiyyətlərinin və həmçinin inanclarının təsir altına düşməsinin qarşısını ...
  • Nini maana ya Feminism?
    15423 Sheria na hukumu 2012/05/23
    Neno (Feminism) linatokana na lugha ya Kifaransa ambalo asili yake ya Kilatini ni (Femind), neno hili hutumika katika lugha mbali mbali huku likiwa na maana moja inayomaanisha uke au jinsia ya kike, ijapokuwa neno hili linapotumika kutoka lugha moja kwenda nyengine huonekana kuwa na mabadiliko kidogo ya ...

YALIYOSOMWA ZAIDI