Uislamu umekuja kwa ajili ya kuwapangia wanaadamu mfumo maalumu wa sheria za kijamii, sheria ambzo ni kwa ajili ya kuweka uhusiano salama na wenye mafanikio baina yao wenyewe kwa wenyewe, baina yao na Mola wao na baina yao na viumbe vyengine vilivyo hai na visivyo hai ulimwenguni. Na lengo hasa lilikuwa ni kuwaweka wanaadamu pamoja na viumbe wengine, kwenye mfumo maalumu kwa ajili ya kuboresha maisha yenye malengo maalumu yaliyo kusudiwa na Mola Mtakatifu.
Mwanachuoni maarufu aliyejulikana kwa jina la Shahidus-Sadri (r.a) anasema kuwa: (ili malengo ya Usilamu yakamilike ipaswavyo, Uislamu ulilazimika kuyadhamini malengo hayo kupitia mambo mawili, nayo ni:
- Mdhamini wa nje: naye ule mfumo na nidhamu yenye kudhamini utendekaji wa sheria hizo ndani ya jamii. Na nidhamu hiyo hukamilika chini ya uongozi wa kiongozi maalumu mwenye sifa ya uadilifu kamili ulio timia.
- Mdhamini wa ndani: naye ni hamu na shauku ilioko ndani ya nafsi, ambayo iwapo watu watakuwa nayo, hapo ndipo wao watakapo zitii sheria na kuzitendea kazi sheria hizo kwa uangalifu na matumaini yenye lengo moja.
Kwa bahati mbaya jamii za Kiislamu siku zote hujaribu kukaa nje ya mambo mawili hayo, na hilo ndilo ndilo lililo sababisha wao kuonekana kuwa ni jamii isiokuwa na mfumo maalumu wa uendeshaji, bali siku zote wakawa ni wenye kunyong’onyea duniani. Lakini kwa upande wa ulimwengu wa Ulaya, wao wameweza kuyafanyia kazi mambo mawili hayo, na hatimae wakaweza kuzifikia zile ngazi ambazo leo ni wenye kujisifia nazo.
Kabla ya sisi kuanza kuulaumu Uislamu, nilazima kwaza tufahamu ya kuwa: Uislamu umekuja kwa ajili ya kuboresha mafungamano yaliopo baina yao wenyewe kwa wenyewe, baina yao na Mola wao na baina yao na viumbe wengine. Ule mfumo wa kijamii alio ujenga Mtume (s.a.w.w) kule Madina, ulikuwa ni mfumo wenye kufungamana na sheria maalumu za kijamii uliokuwa na nia ya kutoa mfano bora kwa jamii mbali mbali za wanaadamu. Kwa jinsi ya mtazamo wa Shahidus-Sadri, ni kwamba: Uislamu umekuja kwa ajili ya kuwawekea wanaadamu mfumo maalumu utakao boresha mafungamano tuliyo yataja hapo juu, na ili malengo ya ufumo huo yakamilike kisawa sawa, Uislamu hou ulilazimika kuwaweka wadhamini wawili madhubuti kwa ajili ya kuudhamini mfumo huo na malengo yake, na wadhamini hao ni kama ifuatavyo:
- Mdhamini wa nje: naye ule mfumo na nidhamu yenye kudhamini utendekaji wa sheria hizo ndani ya jamii. Na nidhamu hiyo hukamilika chini ya uongozi wa kiongozi maalumu mwenye sifa ya uadilifu kamili ulio timia.
- Mdhamini wa ndani: naye ni ile hamu na shauku ya nafsi za wanajamii juu ya kutaka kutenda matendo yao chini ya misngi hiyo ya sheria wanayo takiwa kuifuata. Na shauku hiyo iliomo ndani ya nafsi zao, ndiyo itakayo wapa wao msukumo wa kushikama na sheria hizo kikamilifu.
Nchi za Ulaya leo ni zenye kiwango kikubwa cha maendeleo yenye huduma bora mabli mbali za jamii, na hali ya kuwa wao walilisoma hilo kutaka katika mfumo wa jamii ya za Kiislamu zilizopita. Baada ya watu wa Ulaya kuanza miamko ya kielimu katika kupingana na mfumo wa kanisa ulio wazorotesha na kuwakandamiza kwa miaka mingi, ghafla wakavamiwa na nguvu za Kiislamu zilizokuwa na nia ya kuleta mabadiliko ulimwenguni kwa ajili ya maendeleo ya wanaadamu. Waislamu walizilingani nchi mbali mbali na kuzifikishia ujumbe wa Uislamu, na kwa bahati mbaya wao waliwajibika kwa namna moja au nyengine kukabiliana na nguvu za kidhalimu kutoka pande tofauti, jambo ambalo lilisababisha kupatikana mapambano ya pande mbili. Katika zama zile Wislamu walikuwa bado ni wenye kushikamana na nidhamu madhubuti za kijamii walizo jifunza kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w). Na baada ya watu wa Ulaya kuuona mfumo na nidhamu ya kijamii ilioko katika Uislamu, wao walianza kutafuta chanzo na sababu ya kuwepo kwa nidhamu iliyo sababisha kuwepo kwa umoja madhubuti ndani ya jamii wa Kiislamu. Na kabla ya hapo Wamagharibi hawakuwa na mfumo mwema wa uongozi wala nidhamu iliyo nyooka ndani ya jamii zao, bali wao walichifunzo nidhamu bora kutoka katika Uislamu, na hatimae wakafanikiwa.
Ni muhimu pia kufahamu kuwa wele wasio fungamana na dini, wao huwa wanashikamana na sheria kupitia dhamana dhahiri za kidunia tu, yaani wao huwa ni watiifu wa sheria kwa kutokana na serikali zao kuwalazimisha kuwa katika hali hiyo, na wala wao huwa hawazielekei sheria hizo kwa udhati wa nyoyo zao, kwa hiyo linalo wafanya wao kuzitii kanuni, ni kule kuwepo mdhamini mkali wa kuzilinda seria hizo, na kule kukabiliwa na jazaa kali yule aendae kinyume na sheria za nchi, ndiko kunako wasukuma wao katika kushikamana na sheria za nchi, na pale tu mdhamini wa sheria anapo pwaya, basi tayari utaona uhalifu umesha zagaa kila sehemu. Hiyo basi ni dalili tosha inayo onesha kuwa wao ni watiifu wa kanuni dhahiri tu. Na jengine linalo wafanya wao kujifunga na kanuni zao, kule kutafuta maslahi ya kidunia, hii ni kwa kutokana na wao kuto kuwa na imani itakayo walazimisha kuzitii sheria hizo kwa sababu ya kutaka maslahi ya baadae (Akhera), kwa hiyo kila mmoja hupingana na tendo la wizi na uhalifu kwa kutoka na kutaka amani ya kijamii ya hapa dunianai, pia yeye huwatendea wengine mema kwa kuwa yeye vile vile anawahitajia wengine wamtendee mema. Kuna mengi ya kuzungumza kuhusiana na suala hili, lakini mimi nitakupa mfano mmoja kuhusiana na hilo, hebu jaribu kusafiri katika msimu wa baridi uelekee Europe, katika msimu kama huo, utawaona madereva wakifuata kanuni za barabarani kisawa sawa, lakini kwa kutokana na barafu ambazo huwa zimetanda barabarani, msongomano wa magari huwa ni mkumbwa, kwa hiyo wao hubidi kusimama pale ziwakapo taa nyekundu kwa muda mrefu zaidi, na pale muda wa makazini unapokaribi kuingia, kila mmoja miongoni mwao utamuona amesha anza kuangalia saa yake, baada muda si mrefu tayari mmoja mmoja utamuona amesha anza kuchomoka na kukiuka sheria. Hilo linatokana na yeye kufanya hisabu za hasara anazowe kuzipata, kwani iwapo yeye atakiuka sheria basi atabigwa faini ya Dola 50, lakini iwapo yeye atachelewa kazini, hapoi yeye atatozwa faini ya Dola 100 na mkuu wake wa kazi. Kipimo cha Wamagharibi katika utendaji wao, huwa kinajidhatiti kupitia faida na hasara za kidunia tu, yaani wao mambo yote huwa wanayaagalia kwa jicho la kidunia, na msingi wao mkuu wa utendaji, huwa umelelema kwenye faida na hasara za duniani peke yake.
Jambo ambalo Uislamu ulitaka kutulea nalo, ni kule sisi kujidhatiti kisheria katika matendo yetu ya kila siku, na wala Uislamu haukututaka sisi tujidhatiti na sheria zetu za Kiislamu kidhahiri tu (kwa kutokana na kukhofia kukabiliwa na sheria), Uislamu haukuwataka Waislamu kuzitii sheria, kwa kutokana na kuwepo polisi anaye wasimamia na kuwapandisha mahakamani, bali uliwataka wawe watiifu wa sheria kwa kule kuwa na imani ya kuwepo kwa Mungu anaye shuhuidia matendo yao, na kwa kutokana na wao kuwa na matumaini ya radhi za Mola wao, huku wao wakitambua vyema kuwa malengo ya sheria hizo ni kwapa wao kile kipaji chao halisi wanacho stahiki kupewa. Na hilo ndilo alilo lifanya Mtume Muhammad (s.a.w.w), Yeye kwa muda wa kipindi kifupi tu cha miaka kumi, aliweza kuwabadilisha mabedui wa Kiarabu walikuwa wakiishi kupitia nguvu za kula nikule, na kuwaweka katika nidhamu madhubuti iliyo wakweza wao kiimani, kistaarabu na kiuchumi, kupitia mafunzo na mfumo maridadi wailojifunza kutoka mbinguni kupitia Mjumbe wa Alla (s.w). Lile basi lililo tukosesha mimi na wewe maendeleo, ni kule sisi kujiona ni werevu zaidi, na ni wajanja zaidi katika kutunga sheria zenye nia ya kujitafutia maendeleo kupitia mikononi mwetu wenyewe. Hilo ndilo lililo tuponza na kutufanya leo kulala na kuwabembeleza Wazungu waje kutusidia. Ya Rabi Mola tuhidi na vichwa vya wakaidi.