Please Wait
KAGUA
22325
Tarehe ya kuingizwa: 2008/09/17
KODI YA TOVUTI fa3363 NAMBARI YA HIFADHI 17735
Group Sheria na hukumu,جنابت,قضای روزه و کفارات
STIKA fidia|janaba|adhana|kulipa|Ramadhani
Summary Maswali
iwapo mtu ndani ya usiku wa mwezi wa Ramadhani atabakia na janaba hadi wakati wa adhana ya asubuhi kwa makusudi bila ya kukoga, mtu huyo atatakiwa kufanya nini? Je ailipe ile siku moja tu, au pia atatakiwa kulipa fidia?
SWALI
nini hukumu ya mtu aliyebakia na janaba ndani ya wezi wa Ramadhani, hadi akafikiwa na adhana ya asubuhi, lakini yeye akaamua kuendelea na funga yake, je hukumu yake itakuwa ni kuilipa ile funga yake moja tu, au pia atawajibikiwa kulipa aina fulani ya fidia kwa tendo lake hilo?
MUKHTASARI WA JAWABU

iwapo mtu atawajibikiwa kufunga mwezi wa Ramadhani, naye kwa makusudi akabakia na janaba hadi adhana ya asubuhi, anaweza yeye akatayamamu katika nyakati za mwisho kabisa kabla ya kuadhiniwa adhana hiyo badala ya kuoga, kwa kuwa wakati wa kuoga haupo tena, kisha aendelee na funga yake, na funga hiyo itakuwa ni sahihi, ingawaje yeye atakuwa amefanya kosa kwa kule kubakia na janaba hadi wakati huo bila ya kuoga. Ama iwapo yeye atakuwa hakuoga, na akawa amefanya hivyo kwa makusudi, na kutayamamu pia akawa hakutayamamu, hapo funga yake itabatilika (itaharibika), na atawajibika kuifunga funga hiyo kwa kuilipa na pia atatakiwa kutoa fidia.[1]

 


[1] Taudhihul- Masail, kilichoshereheshwa na Imam Khomeiniy, juz/1, uk/908, suala la 1619, lisemalo: iwapo kwa makusudi mtu atabakia na janaba hadi adhana ya asubuhi bila ya kukoga, apia iwapo wadhifa wake ukawa ni kutayamamu lakini pia akawa hakutayamamu, huyo atabatilikiwa na funga yake. Pia rejea kitabu Ajwibal- Istiftaat, juz/1, uk/133.