Please Wait
13259
Msichana na mvulana wanaweza kuwa na aina mbali mbali za mahusiano ndani ya jamii ya wanaadamu, na bila shaka baadhi ya mahusiano hayo huwa si mahusiano salama na si halali. Kwa kweli swali lililo ulizwa na muulizaji wetu, ni swali lisilokuwa la wazi, lakini sisi tutalijibu swali hili kupitia aina mbali mbali za mitazamo, kwa jinsi ya makadirio ya jawabu yanavyoweza kukadirika kielimu na kiakili.
Maelezo ya Hadithi kuhusiana na mahusiano ya mvulana na msichana:
1- Katika kitabu kijulikanacho kwa jina la (Usulil-Kafi), kuna Riwaya iliyopokewa na As-a’d Al-Askaaf kutoka kwa Imamu Baaqir (a.s) isemayo kuwa: (Siku moja kijana miongoni mwa vijana wa kiansari alikuwa akitembea kwenye chochoro za mji wa Madina, na mara akakutana na mwanamke, na katika zama zile wanawake walikuwa wakivaa hijabu zao hadi kufia chini ya masikio yao tu. Baada ya mwanamke yule kutangulia mbele kidogo, yule kijana alianza kumfuata hadi akafikia kwenye kichochoro ambaco kilikuwa ni chembamba mno, na yeye alipokuwa akiendelea kumfuata ndani ya kile kichochoro, mara uso wake ukakwama kwenye kitu fulani kilichokuwa kimekamatana na ukuta wa kile kichochoro, naye bila ya hata kuhisi maumivu aliendelea kumfuata yule mwanamke, na baada ya yule mwanamke kutoweka, mara yeye akatanabahi kuwa anavujwa na damu kutoka usoni mwake na kumwagikia kwenye sehemu ya kifuanai mwa nguo zake, hapo alijisemeza mwenyewe kwa mwenyewe kwa kusema: naapa kwa Mola, ni lazima niende kwa Mtume (s.a.w.w) na kumhadithia tokeo hili. Na pale Mtume (s.a.w.w) alipomuona akiwa katika hali kama ile, alumuuliza: umesibiwa na nini? Hapo yule kijana akamhadithia Mtume (s.a.w.w) yale yaliyomtokea, na baada ya hapo Jibrail akashuka na Aya isemayo:[1]
(قُلْ لِلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا مِنْ أَبْصارِهِمْ وَ يَحْفَظُوا فُرُوجَهُمْ ذلِكَ أَزْكى لَهُمْ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِما يَصْنَعُونَ).
Maana yake ni kwamba: (Waambie waumini kuwa wainamishe macho yao chini, (na waisiwaangalie wanawake wasioruhusiwa kuwa na mahusiano nao bila ya kuwepo masharti maalumu), na wazihifadhi tupu zao, kwani hilo ni takaso kubwa kwao, kwa hakika Mwenye Ezi Mungu ni Mjuzi wa yale wayatendayo (waja wake)).[2]
2- Mtume (s.a.w.w) amesema: (Siku ya Kiama macho yote yatalia ispokuwa macho ya aina tatu, nayo ni: jicho linalolia kwa ajili ya kumkhofu Mwenye Ezi Mungu, jicho linaloepu kuyaangalia yale yaliyoharamishwa kuyaangali, (kutomuangalia mtu kwa nia mbaya na ya haramu) na la tatu ni lile jicho linalobaki macho ( wakati wa usiku huku wengine wakiwa wamelala ) kwa ajili ya kumuabudu Mola).[3]
3- Imamu Ridhaa (a.s) amesema: (Ni haramu kwa waumini kuziangalia nywele za mwanamke aliye olewa au asiye olewa, hii ni kwa sababu ya kuwa jambo hilo ni lenye kuziamsha shahawa zao na kuwasogeza wao kwenye maasi).[4]
Maswali yenye kufungamana na swali hili ni:
Swali namba 1044, na kwenye tovuti ni namba 1110.
Swali namba 6669, na kwenye tovuti ni namba 6745.
[1] Tarjama ya kitabu Al-Miizaan, cha Muhammad Husein Tabaatabaai, juz/15, uk/160, chapa ya Islamiy, Qum, mwaka 1374 Shamsia.
[2] Suratun-Nuur, Aya ya 60.
[3] Kanzud-Daqaaiqi-wa-Bahrul-Gharaaibi, cha Muhammad Mahdiy, juz/9, uk/278, chapa ya Wizaarate Irshaad, Tehran, mwaka 1368 Shamsia.
[4] Bihaarul-Anwaari, cha Muhammmad Baaqir Majlisiy, juz/101, uk/34, chapa ya Daarul-Wafaa, Beirut.