Please Wait
7960
Ofisi ya Ayatullahi Sistani (Mungu ameweke) inajibu kwa kusema:
Iwapo wewe ulikuwa hujui kuwa saumu ni wajibu, basi lipa tu hizo funga za miaka minane, na hakuna haja ya kuzilipia fidia.
Ofisi ya Ayatullahi Makaarim Shiraziy (Mungu amuweke) nayo inajibu kwa kusema:
Anza kuzilipa sala na funga kidogo kidogo, na kuhusiana na ulipaji wa fidia juu ya funga hizo, rejea katika kitabu chetu Taudhihul-masaail, kwenye suala la 1401 hadi 1402, na lile ambalo litakuwa liko nje ya uwezo wako, Mola atakusamehe.
Ofisi ya Ayatullahi Safi Gulpeigani nayo iasema:
Iwapo utakuwa wewe ulikuwa ukijua kuwa saumu ni wajibu kwa yule aliyefikia baleghe, kisha ukawa unajuwa kuwa mwanzo wa baleghe ni kuanzia umri gani, hapo utawajibikiwa kuzilipia fidia saumu hizo pamoja na kuzikidhi.
Jawabu kutoka kwa Ayatullahi Mahdiy Hadawiy Tehraniy (Mungu amlinde):
Hukumu ya mtu ailyekula kwa makusudi, ni kufunga siku sitini mfullulizo au kuwalisha mafakiri sitini kwa kila siku moja ambayo umekula. Iwapo mtu atataka kutoa kafara (fidia) ya funga ya siku moja, itambidi ampe fakiri kiwango cha gramu 750 za chakula, kama vile ngano, mchele au kile chenye kufanana na vitu kama hivyo.