Please Wait
10331
Wanazuoni wamekhitalifiana kuhusiana na suala hilo. Kwa kupata jawabu tosha, ni lazima utuambie kuwa wewe ni mfuasi wa mwanazuoni gani? Ili tuweze kukupa jawabu makini zaidi. Kwa vyovyote vile mitazamo ya baadhi ya wanazuoni wetu ni kama iuatavyo:
Bahjat (r.a) na Khameneiy (Mungu amuhifadhi), wanasema: iwapo sindano hizo zitakuwa ni kwa ajili ya lishe au zitakuwa na aina fulani ya lishe, basi ni bora kua na tahadhari nazo na kujiepusha nazo, lakini zitapokuwa ni kwa ajili ya dawa au kwa ajili ya ganzi, basi hakutokuwa na tatizo kuzitumi sindano hizo.
Fadhil Lankarani (r.a) naye anasema: mwenye saumu anatakiwa kujiepusha na sindano na maji ya kutia nguvu mwilini, lakini hakuna tatizo kupiga sindano za dawa au za ganzi katika hali ya saumu.
Makari Shirazi (Mola amhifadhi) naye anasema: kwa kuchukua hadhari ya kutoharibika funga, ni lazima mtu ajiepushe na sindano za kutia nguvu pamoja na za dawa, pia asitumie maji ya lishe ambayo yanaingizwa kwa mirija maalumu mwilini, lakini hakuna tatizo kutumia sindano za ganzi.
Mwana chuoni Jawadi Tabrizi, Safi Gulpeigani, Nuru Hamadani, Wahidi Kurasani pamoja Sistani wanasema: sindao yeyote ile haiwezi kubatilisha saumu, ewe ni ya kutia nguvu na lishe au ni kwa ajili ya dawa.[1]
Jawabu kutoka kwa mwanazuoni Ayatullahi Mahdi Hadawiy Tehraniy (Mungu amuhifadhi) ni kama ifuatavyo:
Piga sindano za nguvu (lishe) pamoja na kutia maji ya lishe au ya nguvu mwilini, ni vitu vilivyoko nje ya hukumu ya kula na ya kunywa, ingawaje ni vizuri mtu kujiepusha na aina hiyo ya sindano pamoja na maji ya nguvu au ya lishe.
Kwa ajili ya kupata faida zaidi rejeo zifuatazo ndani ya tovuti hii:
1- funga na utumija wa dawa, swali la 2986 (tovuti: 3479).
2- kutumia spray katika hali ya saumu, swali la 5845 ( tovuti 6063).
[1] Taudhihul-Masail Maraaji, ju/1 uk/892 suala la 1576. Ajwibatul- Istiftaat cha Ayatullahi Khameneiy swali la 767. Taudhihul-Masail cha Ayatullahi wahid Khurasaniy, suala la4851.