Please Wait
8752
Suala la kuonekana kwa mwezi ni lenye umuhimu ndani ya miezi yote, lakini suala hilo huwa ni lenye kupewa kipau mbele zaidi ndani ya mwezi wa Ramadhani, kwa kutokana na ulazima wa ibada ya funga iliyomo ndani yake, ambayo ni ya wajibu kwa Waislamu wote, pia suala hilo huwa na umuhimu kwa kutokana na uharamu wa kufunga saumu ndani ya siku ya Idi. Kwa hiyo si ndani ya mwezi wa Ramadhani tu watu huwa ni wenye kulizingatia jambo hilo, bali suala hilo hupewa kipau mbele pia katika mwezi wa Dhul- Hijja, kwa kutokana na ile ibada ya hija. Ndani ya miezi kama hiyo utawaona Waislamu wameshughulika sana katika kulifahamu suala la kuandama kwa mwezi, ili waweze kufahamu kuwa je tayari wameshawajibikiwa na ibada hiyo au la? Na kinachooneka hapo ni ile hali ya mtu kujihisi kuwa na uzito fulani ulioko juu ya shingo yake ndani ya miezi fulani, miezi ambayo mja huwa anakabiliwa na aina maalumu ya ibada, hali ya kuwa suala hilo huwa halipo ndani ya miezi mingine, na wala mtu huwa hajihisi kuwa na uzito fulani juu ya shingo yake ndani ya miezi iliyobakia. Na hata ndani ya mwezi wa Muharram, mtu huwa hajihisi kuwa ni mwenye jukumu mbele ya Mola wake, kwa kule kuitanguliza au kuichelewesha siku hiyo, yaani iwapo mtu atataka kuliadhimisha jambo fulani ndani ya mwezi fulani, huwa yeye hajihisi kuwa ni mwenye jukumu la kuitambua kwa makini siku ya kuliadhimisha jambo hilo.