Please Wait
7679
- Shiriki
Wanazuoni wote wa Kifiqhi wanasema kuwa: ni wajibu wa kila mwenye funga kuchukuwa tahadhari, na kutofikisha kitu chochote kile kama vile tumbaku au moshi wa sigara ndani ya koo yake.[1]
Na hakuna hata mmoja miongoni mwa wanazuoni aliyetoa ruhusa ya kuvuta sigara ndani ya funga, kwa hiyo basi ni lazima mtu anayefunga saumu ajizuie na vitu vyote ikiwemo sigara na nyenginevyo, tokea mwanzo wa adhana ya alfajiri hadi adhana ya magharibi. Ni jambo lililo wazi kuwa, iwapo mtu atavuta sigara, basi funga yake itaharibika na atatakiwa kuifunga funga yake pamoja na kuilipia fidia kama ilivyo fafanuliwa kwenye vitabu vya sheria za funga.[2]
[1] Taudhihul-Masaail cha Imam Khomeiny, juz/1, uk/903.
[2] Taudhihul-Masaail cha Imam Khomeiny, juz/1, uk/928, suala la 1660, linasema: mtu atakayewajibikiwa kuilipia fidia funga yake, huyo atatakiwa kumwachia mtumwa huru, au kama ilivyoelezewa mahala pake, kuwa aweza pia kufunga miezi miwili mfululizo, au awalishe maskini sitini, au akitaka anaweza kumpa kila mmoja kiwango cha nafaka cha kumfidia chejio chake, ambacho ni kiasi cha gramu 750 za ngano au kinachofanana nazo, na kama hana uwezo wa hilo, basi atowe kiwango ambacho atakuwa na uwezo nacho na awape maskini, na ikiwa pia hilo hana uwezo nalo, hapo anatakiwa atubie kwa Mola wake kwa kusema ((استغفر اللَّه.Na ni muhimu kwake kuihadhari adhabu ya Mola wake, hivyo basi wakati wowote ule atapopata uwezo, anatakiwa kulipa fidia ya funga hiyo.
Njia pekee ambayo mtu wa aina kama hii anaweza kuitumia ili afunguwe funga yake, ni kusafiri kwa kiasi cha masafa ya kilomita 22/5, hapo ndipo ataposalimika na fidia za kuilipa funga yake kwa mtindo uliotajwa hapo juu, na katika hali kama hiyo, yeye atatakiwa kulipa siku moja ambayo amekula kwa sababu ya kuwepo safarini.