advanced Search
KAGUA
6986
Tarehe ya kuingizwa: 2018/01/24
Summary Maswali
Tafadhali naomba munieleweshe, nini maana ya hijja kilugha?
SWALI
Tafadhali naomba munieleweshe, nini maana ya hijja kilugha?
MUKHTASARI WA JAWABU
Hijja kilugha; Ni kukisudia na kukiendea kitu au jambo fulani.[1]
Neno hijja Kisheria na kitaalamu; Neno hijja kisheria ni lenye kuashiria aina maalumu ya ibada yenye kutendeka mahala maalumu, kwa mfumo na wakati maalumu. Ibada hii inatakiwa kutendeka katika nyumba maalumu ya Mwenye Ezi Mungu iliyopo Makkah. Ibada hii inatakiwa kufanyika kwa nia ya kujikaribisha na kujisogeza kwa Mola Mtukufu.[2]
Kuna fungamano kubwa baina maana ya neo hijja kilugha na kisheria (kitaalamu), kwani mtu mwenye kutaka kufanya ibada ya hijja ni lazima aikusudie na aiendee nyumba ya Mwenye Ezi Mungu (Kaaba) ilioko Makka.

Twataraji utaridhika na jawabu hii.
Ahsante.
 

[1] Rejea kitabu: Jamharatul Lughah/juz 2/ Uk 86/ cha Muhammad bin Hussein Ibnu Darid/ Chapa kwanza ya Darul I’lmi lilmalayiin Beirut. Rejea kitabu: Mu’jamu Maqayisil Lugha cha Ibni Faris /Juz 2/Uk 29/ Chapa ya kwanza ya Maktabatul Ii’lam Al-islami/ Qum Iran/ Chapa ya mwaka 1404 Shamsia. Pia kwa ufafanuzi zaidi, unaweza kurejea kamusi mbali mbali za lugha ya Kiarabu.
[2] Rejea kitabu: Al-qamusul Fiqhi Lughatan wa Istilaha/ Uk 76-77/ Cha Abu Jaibi Saa’di/ Chapa ya pili ya Damascus iliyochapwa na taasisi ya Darul Fikr. 
TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI