Please Wait
13372
- Shiriki
Ndani ya fatwa za wanazuoni, kuna mambo 9 ya msingi yenye kubatilisha saumu, nayo ni: 1- kula na kunywa, 2- kujamii, 3- kupiga ponyeto, 4- kumzulia uongo Mola na Mtume wake pamoja na maimamu (s.a.w.w), 5- kuingiza vumbi zito kooni, 6- kuzamisha kichwa majini, 7- kubaki na janaba, hedhi au nifasi hadi wakati wa adhana ya asubuhi, 8- kutumia aina fulani ya ulevi na la 9- ni kutapika.[1] Mambo tisa yaliyotajwa hapo, yote ni yale mambo yenye kubatilisha saumu, na siyo mambo ambayo ni haramu kuyatenda ndani ya mwezi wa Ramadhani. Hivyo basi iwapo mke na mume watakuwa wako nje ya saumu, wanaweza kulala pamoja. Lakini Wanazuoni wa kifiqhi, wamesema kuwa: kufanya hivyo ni makruhu (aipendezewi) kwa yule asiyekuwa na saumu, na hukumu ya tendo hilo kwa wale wasiokuwa na saumu ni makruhu.[2]
[1] Taudhihul-Masaail kilicho shereheshwa na Imam Khomeiniy, juz/1, uk/891, suala la 1572, kilochapishwa na Muasasatu Nashru Islamiy, kitengo chenye fungamano na Jamiatul-Mudarrisiin, Qum, chapa ya nne ya mwaka 1424 Hijiria Qamaria.
[2] Taudhihul-Masaail kilicho shereheshwa na Imam Khomeiniy, juz/1, uk/955.