Please Wait
10752
- Shiriki
Kwa kweli kisheria hakuna matatizo yoyote yale kuhusiana na suala hilo la mtu kuwa na aina mbili za kazi au madaraka. Ndio Uislamu umewatahadharisha watu kuhusiana na kuwa na mapenzi makubwa ya kuipenda dunia na kuyasahau maisha ya Akhera, dlakini mtu anaweza akawa na aina mbili za kazi huku yeye pia akawa ni mcha Mungu, na kwa upande mwengine, yawezekana mtu akawa na kazi na madaraka mamoja tu, lakini yeye akawa ni mpezi wa maisha ya kidunia kupita budi. Hapa sisi tunaweza kusema kuwa: wakati mwengine huwa ni jambo la wajibu na lazima mtu kuwa na madaraka au shughuli za aina mbili, kwani wakati mwengine kipato anachokipata kutoka katika kazi yake, huwa hakiwezi kukidhi mahitajio ya maisha yake ya kibinasi na kifamilia, katika hali kama hii hii basi mtu huwajibikiwa kutafuta kazi ya pili kwa ajili ya kukidhi mahitajio hayo.
Kwa upande wa sheria na kanuni serikali ndani ya jamii mbali mbali, kila nchi huwa na hukumu yake ya kisheria kuhusiana na swali lako hili, lakini pia tunatakiwa kufahamu kuwa: suala la mtu kushika aina mbili za madaraka, linaweza kumsababishia yeye kutoweza kuzitekeleza kazi zake kimakini na kikamilfu. Na wakati mwengine kule mtu kuwa na kazi mbili kunaweza kumsababishia yeye asiweze kumudu kisawa sawa kazi zake za msingi, kama vile kazi za malezi na kuishughulikia familia yake kisawa sawa, katika hali kama hiyo yeye hatoruhusiwa kushika kazi na nyadhifa za aina mbili. Hii inatokana na kule shria kuyazingatia maniufaa kamili ya mwanaadamu kibinafsi na kijamii, kwa hiyo sheria haiwezi kumvumilia mtu anayevuruga maslahi msingi ya maisha yake au jamii yake kwa utashi wa kujitafutia maslahi bora zaidi yasiyo ya msingi kama vile kipato au madaraka na uluwa. Kwa kutokana na kuwa, kigezo bora na madhubuti kwa wanaadamu ni Mtume wetu Muhammd (s.a.w.w), hebu basi tuiangalie Riwaya kutoka kwa Imamu Husein (a.s) aliyoipokea kutoka kwa baba yake Ali (a.s), Yeye (Imamu Husein (.s)) Amesema: (Mimi nilimuuliza baba yangu kuhusiana na maisha ya Mutme (s.a..w.w), Naye (a.s) akaniambia: Yeye Mtume (s.a.w.w) alikuwa akirudi nyumbani kwake kwa hiyari yake mwenyewe na hakuwa akisukumwa na au kuvutwa na mtu fulani, Naye (s.a.w.w) alikuwa akiugawa wakati wake sehemu tatu: sehemu moja ni ya ibada, sehemu ya pili ni ya familia yake na sehemu ya tatu ni yake yeye…)[1]
[1] Ibara ya Hadithi hii kwa lugha ya Kiarabu ni kama ifuatavyo:
"قال الحسين عليه السّلام: سألت أبي عن مدخل رسول اللّه صلّى اللّه عليه و آله، فقال: كان دخوله في نفسه مأذونا في ذلك، فاذا آوى إلى منزله جزّى دخوله ثلاثة أجزاء: جزءا للّه و جزءا لأهله و جزءا لنفسه ..."
Tarjama ya Sunanun-Nabiy, cha Allaama Tabaatabai, juz/1, uk/15 na 19, ya Muhammad Hadi Faqhiy, chapa ya saba ya Kitabu Furuushiy Islaamiyya, Tehran, mwaka 1378 Shamsia.