Please Wait
10818
Neno (Raudha) ni neno maalumu linalotumiwa na waombolezaji wa mwauwaji ya Imamu Husein (a.s), na neno hili linatoka kwenye kitabu maarufu cha maombolezo ya Imamu Husein (a.s), kijulikanacho kwa jina la (Raudhatush-Shuhadaa), na kitabu hichi ni moja kati ya vitabu vya mwanzo vilivyonukuu tokeo la Karbala, na mwandishi wa kitabu hichi ni Molla Husein Kaashifiy Sabzewaariy, maandiko ya kitabu hicho yalitumika kwa muda mrefu katika vikao mbali mbali vya maombolezo, na hilo ndilo lililosababisha maombolezo ya Imamu Husein kuitwa (Raudha).
Katika zama zetu za leo, pale isemwapo (kusoma Raudha), huwa inakusudiwa ule mtindo maalumu wa sauti ya kusikitisha katika kuyasoma maombolezo yenye kuomboleza misiba ya Ahlul-Bait pamoja na Maimamu wote kwa jumla (a.s), jambo ambalo lilieonekana kutiliwa mkazo sana na Maimamu (a.s), kwani jambo hilo moja kati ya mambo muhimu yenye kuzifungamanisha nyoyo zetu na Maimamu hao Watukufu, pia hilo ni moja ya mambo yenye kuihuisha dini ndani ya zama tofauti.
Maana asili ya neno Raudha, ni Bustani, lakini umashuhuri wa maombolezo kutwa Raudha, unatokana na wasomaji wa zama mbali mbali zilizopita kukitegemea kitabu kilichojulikana kwa jina la (Raudhatush-Shuhadaa) kuwa ndio kitabu katika vikao vyao vya maombolezo, na mwandishi wa kitabu hicho ni Molla Husein Kaashifiy. Mlla Husein Kaashifiy aliyefariki mnamo mwaka 910 Hijiria, alikuwa ni mmoja wa wanazuoni na wanamembari maarufu, naye alisifika sana kutokana na sauti yake nyororo aliyokuwa nayo, katika zama za utawala wa Sultani Husein Baiqiraa alielekea katika mjia wa Haraat, ambo ulikuwa ndiyo makao makuu ya Sultani huyo, kwa kutokana na uwezo wake wa kielimu na umaridadi ufahamu wake, pia kutoka na kule kuimudu vyema membari katika utowaji wake wa hutuba, na kwa upande mwengi kuwepo kwa lile shindikizo la sauti yake nyororo, yote hayo yalichangia kumpa yeye umaarufu wa haraka kutoka katika mji huo, na Sultani naye akawa amevutiwa naye mno, na hilo likawa ndiyo sababu ya yeye kuwa na sehemu maalumu ndani ya kifua cha Sultani Husein, na hatimae kimbinga cha sifa zake hizo kikawakumba wale wote waliokuwa karibu na Sulatan na kwaelekeza kwake, wakiwemo watoto Sultani, mawaziri pamoja na wanasanaa. Mwanachuoni huyu ametunga zaidi ya vitabu 40. Moja kati vitabu vilivyotungwa na mwanachuoni huyu, ni kile kitabu maaru kijulikanacho kwa jina la (Raudhatush-Shuhada), ambacho alinukuu ndani yake tokeo la Karbala kwa kupiti lugha ya Kipashia.
Kitabu hicho kilikuwa na mtindo maalumu uliyoyapamba maombolezo ya Imamu Husein (a.s), na kuyafanya yakolee huzuni zaidi, jambo ambalo liliwafanya wengi miongoni mwa wasomaji wa maombolezo kukitumia kitabu hicho moja kwa moja katika vikao vyao vya uombolezaji. Na baada ya kupita muda mrefu huku wao wakikisoma kitabu hicho, mwishowe wao wakaweza kuyahifadhi maandiko ya kitabu hicho, nao wakaanza kuomboleza bila ya kukishika kitabu hicho mkononi. Minamo Karne ya kumi Muhammad bin Suleimaan Fudhuuliy akakitarjumu kitabu hicho kutoka kwenye lugha ya Kipashia na kukipeleka katika lugha Kiturki.[1]
Hiyo basi ndiyo sababu kuu iliyosababisha maombolezo ya Maimamu (a.s) kupewa jina (Raudha).
[1] Kwa ajili ya uhakiki zaidi, rejea kitabu Farhange Ashura, cha Jawad Muhaddithiy, uk/189, chapa ya Ma’aruuf, Qum, Mwaka 1374 Shamsia. Pia rejea kitabu Negareshe Irfaaniy Falsafiy wa Kalaamiy be Qiyaame wa Shakhsiyyate Imamu Husein (a.), cha Qaasim Turkhaan, uk/470, chapa ya Chelcheraagh, Qum, mwaka 1388 Shamsia.