Please Wait
11870
Kilugha panapotumika neno Imani au itikadi, humaanisha kule mtu kukubali na kusadiki, na maana hii huwa ni kinyume cha neno kukadhibisha na kukanusha. Kitaalamu neno imani huwa linamaanisha kule mtu kusadiki na kuamini jambo fulani kimatamshi, kimoyo pamoja na kimatendo, lakini neno utulivu ambalo ni tafsiri ya neno "اطمینان" lililoko kwenye lugha ya Kiarabu, huwa linamaanisha ile hali kupoa kwa moyo na kupata utulivu na kuepukana na fazaa zilizo ukumba moyo huyo kabla ya utuivu huo.
Tofauti baina ya imani na utulivu
Pale mtu fulani anapotatizwa na jambo fulani, yawezekana yeye akatumia dalili na njia za kimantiki ili ajithibitishie kuwa yeye yuko kwenye ukweli na usawa, na hilo linaweza kuiridhisha akili yake, lakini bado mara nyingi watu wenye kufanya jambo kama hilo, huonekana kuwa nyoyo zao bado ziko katika hali ya wasi wasi. Lakini iwapo moyo wa mtu utakuwa umeridhika na hali halisi ya matokeo au yale mambo yanayomtatiza, au kuridhika na ufafanuzi wake alioutumia katika kulitatua jambo hilo, hapo basi moyo wake utapata utulivu, naye ataepukana na wahaka wa moyo.
Tanapoziangalia Riwaya mbali mbali, tutakutia kuwa: moja ya yale maswali aliyoulizwa Imamu Ridhaa (a.s), lilikuwa ni kuhusiana na suala hili ambalo sisi tumo katika njia ya kulitafiti na kulipatia jawabu, ndani ya moja miongoni mwa Riwaya hizo, Imamu aliulizwa swali lifuatalo: (Je hivi Nabi Ibrahim (a.s) alikuwa na shaka fulani moyoni mwake? Imamu Ridha (a.s) alijbu kwa kusema: hapana, bali Nabi Ibrahim (a.s) alimuombo Mola wake amzidishie yakini zaidi, ili iwe ni nyongeza juu ya ile yakini yake aliyonayo).
Neno imani kilugha huwa lina maana ya kusadiki, ambako huwa ni kinyume cha neno kukanusha,[1] na kitaalamu neno hili huwa lina maana ya kukiri na kukubali kwa matamshi, pamoja na kuwa na fungamano la imani hiyo kimoyo, vile vile kutenda matendo yaendayo sawa na imani hiyo ilivyo.[2] Ama neno "اطمینان" ambalo kwa Kiswahili ni lenye maana ya utulivu, kilugha huwa linaaanisha kupoa na kupata utulivu wa moyo au utulivu wa roho, baada roho au moyo huo kukumbwa na wahaka.[3]
Tofauti baina ya imani na utulivu wa moyo
Kuna baadhi ya wakati sisi huwa tunajaribu kuzikinaisha na kuzikubalisha nyoyo zetu kutokana na mambo fulani yanayotukereketa, mabadilisho ambyo huwa tanayafanya kupitia dalili za liakili na kimantiki, ili kuzifikia yakini na imani fulani ambazo sisi tayari tumesha amua kuzikubali na kujifunga nazo, lakini pia wengi miongoni mwetu huwa bado mioyo yao na roho zao zina wahaka na hazijaridhika na dalili hizo za kiakili au kimantiki.
Lakini pale sisi tunapokuwa tumeridhika na mambo hayo kupitia nyoyo zetu na kukubaliana na mabo hayo kiroho na kiimani, hapo basi tayari nyoyo zetu tutazikuta kuwa ni zenye kupata raha na utulivu ndani yake. Hali ambayo huziweka mbali nyoyo zetu kutokana na wahaka pamoja na wasi wasi; kwa mfano: sisi sote tunaamini kuwa maiti hawezi kumdhuru mtu na wala hawezi kutendo jambo fulani kama vile kuinuka, kutembea na kadhalika, ama kwa kutokana na wasi wasi tuliokuwa nao moyoni mwetu, kila mmoja wetu huwa ni mwenye kumkhofu maiti, na khofu hiyo huzidi zaidi pale mtu huyo anapokuwa karibu na maiti huyo katika nyakati za usiku huku yeye akiwa peke yake. Lakini kwa upande wa wale watu ambao ni wenye kuwa na mazoea ya kukaa na maiti mara kwa mara, wao huwa hawawaogpi maiti.[4] Kwa kweli moyo wa mtu huwa hautulii hadi pale mtu anapopata yakini kutokana na kile yeye kinachombughudhi au kumtatanisha. Nabii Ibrahim (a.s) alikuwa na imani kamili juu ya ufufuo na kuhuika tena kwa wafu, naye hakuwa na shaka ya aina yoyote ile kuhusiana na hilo, na kule yeye kumtaka Mola wake amuoneshe namna ya vile anavyowahusha na kuwafufua maiti, kulikuwa na nia ya kuifikia yakini kamili ya moyo wake juu ya jambo hilo.
Na katika Riwaya fulani, Imamu Ridha (a.s), aliulizwa na mtu fulani kuhusiana na hilo, na swali hilo lilikuwa ni kama ifuatavyo: je Ibrahim (a.s) alikuwa na shaka moyoni mwake? Imamu Ridha (a.s) alijibu: hapana, bali Ibrahim (a.s) alikuwa na yakini kamili, lakini alichokitaka kwa Mola wake, ni kuitimiza yakini ya moyo wake.[5]
Kuna Riwaya zenye kuonesha ubatili wa moja kwa moja juu ya fikra za wale wenye kuona kuwa: kwa sababu Ibrahim (a.s) alikuwa na shaka kuhusiana na ufufuo kisha akamuomba Mola wake amuoneshe dalili zitakazo utuliza moyo wake, basi na mimi pia nina haki ya kumtaka Mola anioneshe dalili maalumu zitakazonituliza moyo wangu.
Moja kati ya zile Riwaya zenye kuukata moja kwa moja mzizi wa fikra hizi, ni Riwaya ifuatayo:
Siku moja kuna mtu aliye muandikia Imamu Musa Kaadhi (a.s) barua na kumwambia: mimi niko katika hali ya shaka kama vile Ibrahim alivyokuwa na shaka kisha akamuomba Mola wake kwa kumwambia: Ewe Mola; hebu nioneshe vile wewe unavyowafufua viumbe wako! basi mimi pia nina hamu ya kupata dalili kama alivyopata Ibrahim (a.s) kutoka kwa Mola wake! Hapo Imamu (a.s) aliijibu barua ya mtu huyo kwa maneno yafuatayo: Ibrahim (a.s) alikuwa ni muumini, kisha akapenda imani yake izidi na ipee zaidi, lakini wewe ni mwenye shaka na wala bado huko katika imani, na kwa kweli mtu mwenye shaka huwa haipatikani kheri kutoka kwake.[6]
Kwa hiyo mtu anatakiwa aamini na kuikiri misingi ya itikadi na imani pamoja na kuwa na yakini kamili juu ya misingi hiyo, na inabidi mtu azifuate njia za dalili madhubuti zitakazoweza kumsaidia katika kulithibitisha jambo hilo ili yeye ajisafishe na aepukana na shaka juu ya misingi hiyo, na hilo ndilo litakalomuokoa yeye kutokana na vikwazo vya maswali mbali mbali, naye pia anaweza kuwafuata wanazuoni ili kujipatia misingi hiyo kwa kupitia misingi madhubuti ya hoja na dalili imara.
Kwa hali yoyote ile, iwapo mtu atatafakari kwa kiasi fulani na akazisoma Aya za Qurani zenye kuhusiana na misingi ya imani, yeye ataweza kujitosheleza ipaswavyo, na pia atafahamu vyema kwamba: njia madhubuti ya kuepukana na urukwaji wa roho na kutokuwa na utulivu, ni kule mja kuikweza imani yake na kujikita ndani ya imani hiyo kisawa sawa. Pale muumini anapotambua na kudiriki kwamba rehema ya Mola wake ni yenye kumlinda na kumpa himaya, yeye huwa tayari anajihisi kuwepo kwenye ngao ya rehema ya Mola wake, na hilo huwa linamfanya yeye kuepukana na matatizo ya kisaikolojia pamoja na kutokuwa na utulivu wa moyo. Mwenye Ezi Mungu anasema:
" " و لا تهنوا و لا تحزنوا و انتم الاعلون ان كنتم مؤمنین. Maana yake ni kwamba: Msinyong’onyee wala msihuzunike na nyinyi ndiwo mlioko juu iwapo kweli mtakuwa ni waumini. Na Mola katika Aya mbali mbali, amesema wazi wazi kwamba: Iwapo nyinyi wanaadamu mtakuwa pamoja na Mola wenu, basi Mola wenu atakumilikisheni nguvu zote za mbinguni na ardhini, na pia Mola wenu ni mjuzi wa matatizo yenu yote mliyo nayo, Naye ni Mjuzi wa utiifu wenu na imani zenu. Vipi basi mja awe katika himaya kama hii, kisha bado yeye awe na wahaka wa moyo? Bila shaka njia zote zenye kumsababishia mwanaadamu mashaka na wahaka wa moyo huwa ni zenye kukomeshwa kupitia imani imara yenye nia safi.
[1] Lisanul-Arab, cha Muhammad bin Mukrim Ibnu Mandhuur, juz/13, uk/21, chapa ya Daarus-Saadir, Beirut, chapa ya tatu ya mwaka 1414 Hijiria.
[2] Al-Kaafi cha Koleiniy, juz/2, uk/27, chpa ya Daarul-Kutubil-Islaamiyya, Tehran, chapa ya mwaka 1365 Shamsia. Hadithi kutoka kwa Imamu Saadiq (a.s) yenye kuzungumzia suala hili ni kama ifuatavyo:
(الْإِيمَانُ هُوَ الْإِقْرَارُ بِاللِّسَانِ وَ عَقْدٌ فِي الْقَلْبِ وَ عَمَلٌ بِالْأَرْكَانِ،)
Kwa ufafanuzi zaidi rejea swali la 1311 katika tovuti yetu lenye kicha cha habari kisemacho: (sharti za imani na Uislamu), codi na kiungo cha swali tovutini ni: (1343), pia angalia swali la 5382 tovutini humo kicha cha habari kisemacho: (tofauti ya imani na elimu), kodi na kiungo cha swali katika tovuti hii ni: (5651).
[3] Mufradaatu Alfaadhil-Qur-ani, cha Husein bin Muhammad Raaghi Isfahaniy, kilichotarjumiwa na kuhakikiwa na Ghulam Ridha Khosrawiy, chapa ya Murtadhawiy, Tehran, chapa ya pili ya mwaka 1375 Shamsia.
[4] Tafsiri Nemune ya Nasir Mkarim Shirazi, juz/1, uk/330, chapa ya kwanza ya kitengo cha uchapishaji cha Taarikhul-Arabiy, Beirut, mwaka 1412 Hijiria.
[5] Nuruth-Thaqalaini, cha Abdu Ali bin Jum-a’ Aruusiy Huwaiziy, juz/1, uk/330, chapa ya kwanza ya taasisis ya Taariikhul-Arabiy, Beirut, mwaka 1412 Hijiria.
[6] Rejea kitabu kilichopita, juz/1, uk/336.