Please Wait
7105
Sisi swali lako tumelifanyia utafiti, na kulisaka katika maandiko mbali mbali yanayoelezea msiba wa Imamu Husein (a.s), vile vile tumeangalia ndani ya kitabu maarufu kijulikanachoa kwa jina la Luhuuf cha Sayyid Ibnu Taawuus, lakini juhudi zetu zimeishia ukingoni, nasi hatukuweza kupata ithibati yeyote ili kuhusiana na sentensi isemayo: ““kutoka kwa mtengwa kwenda kwa Habibu” ambayo inadaiwa kuwemo ndani ya barua iliyoandikwa na Imamu Husein (a.s) kwenda kwa Habibu bin Madhahir. Nasi bila ya kuwa na ushahidi juu ya suala hilo, hatuwezi kuihusisha na kuiegemeza sentensi na maandiko hayo moja kwa moja kwa Imamu Husein (a.s).
Lakini lile tuliloweza kulifikia ni kwamba, Habibu bin Madhahir alikuwa ni mfuasi mwema na mtiifu wa Imamu Husein (a.s), naye alishiriki vita vya Karbala na kuuwawa katika vita hivyo.[1] Habibu bin Madhahir alikuwa ni miongoni mwa watu waliopata mualiko maalumu wa Imamu (a.s) ya kuwataka wao waje katika mji wa Kuufa uliopo Iraq.[2] Maneno ambayo yamedaiwa kuwa yanatokana na barua ya wito huo wa kumtaka Habibu bin Madhahir kwenda katika mji wa Kuufa ili awe pamoja na Imamu (a.s), si maneno ya Imamu Husein (a.s), bali ni ziada ya wale wenye kusoma mashairi ya taazia, nao wameiengeza ziada hiyo kwa kule kutaka kukithirisha hali ya hisia ya msiba na huzuni ndani ya nyoyo za wasikilizaji wa mashairi hayo, na wala maneno hayo hayatokani na Imamu Husein (a.s).
[1] Tarjama ya kitabu Taarekhet-Tabari ya Kifarsi ya Abul-Qasim Paayande, juz/7, uk/3020, chapa ya tano ya Asatiir Tehran, mwaka 1375 Shamsia.
[2] Tarjama ya kitabu Taarekhet-Tabari ya Kifarsi ya Abul-Qasim Paayande, juz/7, uk/2923.